@transcript kwa huduma za ufasiri na ujanibishaji wa programu za kompyuta

Kwa zaidi ya miaka kumi sasa, tumekuwa wataalamu katika ufasiri wa kiufundi, usimamizi wa miradi ya lugha nyingi na ujanibishaji wa programu za kompyuta.

Sisi ni wataalamu katika ujanibishaji – huo ni ubadilishaji wa programu na nyaraka ziwe na ukubaliano maalum na utamaduni, isimu na kiufundi katika soko linalokusudiwa. Pia tunatoa huduma zinazohusiana na mchakato wa ufasiri, kama vile usimamizi wa maudhui, majaribio kwa kutumia programu za marejeleo zilizojanibishwa, uundaji na udumishaji wa hifadhi za istilahi, na Uchapishaji Ofisini na mchakato wa michoro.
Kwa kawaida, huduma zetu zinaweza kubadulishwa ili zitimize matakwa ya wateja wetu. Zimeundwa kwa vitengo huru vilivyobinafsishwa na vyenye ufanisi wa hali ya juu – ambavyo pia, ukituma ombi, vinaweza vikafungamanishwa kwa usimamizi wa kitaalam.

Tunatarajia kusikia mengi kuhusu kazi yako!